Sunday, August 4, 2024

MFANO WA BARUA YA MAAFISA UTAMADUNI

 Je, unatafuta nafasi ya kazi kama Afisa Utamaduni Daraja la II? Barua hii ya maombi ni mfano mzuri wa jinsi ya kuandaa maombi yako ili kujitokeza kwa waajiri. Itakusaidia kueleza sifa zako na utayari wako kwa ufanisi.

 


KABLA YA KUPAKIA BARUA HAKIKISHA

Umepiga Mihuri ya Mwanasheria kwenye Documents zako

Umewaweka wadhamini wako watatu na kuendelea wa kuaminika

Umeweka Passport size yako yenye Background ya Blue

Umebadilisha Makazi yako ya kudumu na kuweka unayoishi sasa kwani (ndiyo wanatumia kupanga eneo la Interview)


KARIBU



AFISA UTAMADUNI MTARAJIWA,

S.L.P 259,
DODOMA.
4/8/2024

KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
DODOMA.

Ndugu,

YAH: MAOMBI YA KAZI YA AFISA UTAMADUNI DARAJA LA II (CULTURAL OFFICER II)

Husika na kichwa cha habari hapo juu,

Mimi ni kijana wa kitanzania mwenye umri wa miaka 26, nimehitimu Shahada ya Awali ya Fasihi ya Kiswahili kutoka chuo kikuu cha Dodoma. Kutokana na tangazo la nafasi za kazi zilizotangazwa tarehe 3 Agosti 2024 ninaomba nafasi ya kazi ya Afisa Utamaduni Daraja la II (Cultural Officer II).

Nina uzoefu katika shughuli za utamaduni, na ninauwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi na weledi. Nimejihusisha na shughuli za kiutamaduni kwa kufanya kazi kama Afisa utamaduni kipindi cha mafunzo kwa vitendo, ambazo zimenipa ujuzi na mbinu za kusaidia jamii kwa ufanisi.

Ninaahidi kuifanya kazi kwa uaminifu na ufanisi kwa maendeleo ya nchi na Taifa kwa ujumla pia nipo tayari kufika kwenye usaili wakati wowote nitakapohitajika ili kutoa maelezo zaidi kuhusu ujuzi na uzoefu wangu

Naambatanisha na vyeti vyangu vya taaluma ikiwemo na wasifu wangu binafsi.

Wako katika ujenzi wa taifa

 

………………………

AFISA UTAMADUNI MTARAJIWA

0712345678


Kwa msaada wa kufanyiwa kazi ajira portal, tafadhali wasiliana nami kwa namba 0659385219. Namba hii pia inapatikana kwenye WhatsApp: Bonyeza hapa kuwasiliana nami.

kuingia ajira portal 👉 https://portal.ajira.go.tz/home 

No comments:

Post a Comment

Machapisho mengine

MFANO WA BARUA YA MAAFISA UTAMADUNI  Je, unatafuta nafasi ya kazi kama Afisa Utamaduni Daraja la II? Barua hii ya maombi ni mfano mzuri wa j...