APPLICATION 5 ZA MUHIMU KWA MWANACHUO
Habari za wakati huu, leo nimeamua kusogeza mada hii mbele zenu kwani, nimeona watu wengi hasa wanafunzi wa chuo wamekuwa wakishindwa kuamua ni application gani muhimu wanaweza kuzitumia wakati wakiwa chuoni
1. WHATSAPP
Hii ni application ya muhimu sana, ukizingatia chuoni hakuna assemble kama vile Advance hivyo mwananchuo katika simu yake anatakiwa awenayo pia iwe online angalau baada ya masaa kadhaa kwani taarifa za muhimu hutumwa humo
2. XENDER
Hutumika kwa ajili ya kushare material yanaweza kuwa ni document, nyimbo au hata applicatin. hii itakusaidia kupunguza gharama kwani badala ya kudownload utaweza kurusha baadhi ya vitu vizuri kutoka kwa wenzako
3. CAMSCANNER
Inatumika kubadilisha hardcopy kuwa softcopy, badala ya kukaa na makaratasi mengi unaweza kuyascann na ukawa unayasoma kama softcopy nyingine
4.WPS/ PDF
kazi yake ni kufungua document zilizo katika mfumo wa softcopy, pia unaweza kuunda document mpya na kuihifadhi kama vile compyuta ifanyavyo. Kikubwa ni kufanya mazoezi kuitumia kwani kama hautaifanyia mazoezi utajikuta unapoteza kazi ulizoziandika bila hata ya kuzihifadhi. masomo yajayo tutaelekezana kwa undani jinsi ya kuzitumia application hizi
5. CHROME
moja ya application inayomilikiwa na Google, nimeipendekeza hii na siyo nyingine kwasababu inaupekee wake ndani yake mfano unaweza ukawa umeipenda makala fulani unakua huna hata ya kuscreenshoot bali unaweza kudownload na kuiweka kama pdf
SI HIZO TU BALI ZIPO NYINGIILA SIKU YA LEO NIMEPENDA KUKUPATIA HIZO KWANZA
*********KWA MAONI NA USHAURI JUU YA BLOG YANGU USISITE KUTOA MAONI*******




Yako poa kaka
ReplyDelete